Tume ya Ulaya imepiga marufuku wafanyakazi wa Umoja wa Ulaya (EU) kutumia mtandao wa TikTok na kuiondoa kwenye vifaa vyovyote binafsi vyenye programu zinazohusiana na kazi ama la, wafute programu zinazohusiana na kazi ikiwa wanataka kubakiza TikTok.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia Marekani na serikali za Magharibi kupiga marufuku matumizi ya mtandao huo unaomilikiwa na China kwa sababu za kiusalama, kufuatia uhusiano mbaya na Beijing.

Mtandao wa TikTok

Aidha wafanyakazi wameamriwa kufuta programu tumizi hiyo kwenye vifaa vya kazi, na pia kuiondoa na kuifuta kweye vifaa binafsi ili kuwa salama.

Tume imewapa wafanyakazi hadi Machi 15 mwaka huu kufanya hivyo ili kulinda taarifa na kuimarisha usalama wa mtandao

Vipers SC yaomba msaada Young Africans
Thomas Sankara azikwa upya eneo alilouawa