Katika kujiweka karibu na wateja wake uongozi wa Kampuni ya maduka ya ki biashara jijini Dar es salaam (Mlimani City Mall) kwa kushirikiana na maduka yaliyopo ndani ya jengo hilo wamekusudia kufanya maonesho ya mavazi ya nguo kwa rika zote kwenye maduka hayo kwa siku tatu mfululizo..

Meneja mkuu wa bidhaa kampuni ya Mlimani city , Pastory Mroso amesema baada ya kampuni hiyo kufunguliwa novemba 2006 hili litakuwa onyesho la kwanza kwa kushirikisha bidhaa za maduka ya kimataifa pamoja na za asili zinazopatikana ndani ya jengo hilo.

Aidha amsema lengo la kuandaa maonyesho hayo ni kukuza ushindani wa kutoa huduma kwa wateja kutokana na kuwepo kwa maduka mengi ya aina hiyo kwa sasa.

Akieleza mafanikio ya jengo hilo kwa wanahabari leo  Bw. Mroso amesema kwamba kwa muda wa miaka kumi wamefanikiwa kuwa na ukumbi wa mikutano wenye hadhi ya kimataifa  uliotumika  kuendesha  kongamano la uchumi 2010 la kimataifa.

Hata hivyo amewataka watu wote wanaopenda kufanya manunuzi sehemu moja na kwa wakati mmoja waweze kufika kwa siku ya tarehe 17 hadi 19 huku wakiendelea kufurahia burudani pamoja na michezo kwa watoto itakayokuwa ikiendelea.

Katika maonyesho hayo yaliyopewa jina  Mlimani fashion festival yataongozwa na mtangazaji maarufu wa kipindi cha Nirvana Deogratius Kithama yatafanyika kwa siku tatu mfululizo huku wateja wakiendelea kufurahia manunuzi kwa bei ya punguzo na burudani mbali mbali.

Wabunge Ukawa 'wajiengua' baada ya Ikulu kuwazuia kwenda Marekani na kumruhusu wa CCM
Video: NIDA kuwapatia Watanzania wote vitambulisho vya Taifa