Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza mikakatia ya kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Mdami amesema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa.

Upatikanaji wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma” – Rose Mdami

mavazi yawakutanisha Mlimani City mall na wateja wake siku tatu.
Sakata la sukari bado changamoto.