Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi miwili kwa Kampuni ya Swissport Tanzania kuhakikisha inaboresha huduma zake, kinyume chake atafuta leseni ya kampuni hiyo.

Aidha Kampuni hiyo ya Swissport ambayo inashughulikia mizigo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), Dar es salaam imelalamikiwa kwa kushuka kwa huduma zake katika uwanja huo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja huo, amesema kuwa kuna ripoti ameipata hivi karibuni kuwa huduma za kampuni hiyo katika uwanja wa ndege wa (JNIA) si nzuri.

“Nakuomba sana, tunakupa miezi miwili kama huduma yako hukuweka vizuri naomba mamlaka ulete tufute leseni ya huyu bwana, mimi nimepewa mamlaka na kanuni na sheria zipo, kama ukishindwa kutoa huduma hiyo, miezi miwili hukubadilika tutakufutilia mbali,”amesema Prof. Mbarawa.

Hata hivyo, Mbarawa amesema kuwa ni lazima kampuni hiyo ifanye kazi katika uwanja huo pamoja na kampuni zingine na kwamba kama walizoea kufanya kazi kwa mazoea, si kwa wakati huu, hizi ni zama zingine, hivyo lazima wafuate taratibu na kanuni zilizowekwa, vinginevyo ataifuta kampuni hiyo.

Video: Marufuku kutimua wanafunzi vilaza, JPM aonya...
Wizara yamkingia kifua Prof. Muhongo