Mwanamuziki wa Tanzania Mbosso amekuwa na wakati mgumu siku za hivi karibuni hususan baada ya kumpoteza mama wa mtoto wake, Martha Shilole maarufu kama Boss Martha aliyepoteza maisha Septemba 11, 2019 akiwa mwenye umri wa miaka 22.

Kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa baadhi ya watanzania walioguswa na msiba wa Boss Martha mara baada ya kusomewa wasifu wake ambao ulimtaja kuwa hajaacha mtoto zaidi ya familia yake ambapo yeye ametajwa kuwa mtoto wa mwisho.

Mbosso kupitia ukurasa wake wa Instagram amevujisha siri hiyo nzito ambayo kwa miaka mingi yeye na marehemu wamekuwa wakiificha kwa muda mrefu ni kuhusiana na mtoto waliobahatika kumzaa pamoja.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mbosso Khan anayefanya kazi zake za muziki chini ya lebo ya Wasafi amesema haya;

“Licha ya vipingamizi vingi juu ya mimi kuwa na Wewe takribani au ndani ya zaidi ya Miaka Mitano (5) iliyopita, hatukuacha kuonyeshana ni kiasi gani tulikuwa tunahitajiana sana kwenye safari yetu ya maisha , Japo jitihada zetu hazikuweza kufanikisha Mimi na wewe kuwa pamoja … ila mbegu tuliyoipanda vuno letu ulichagua liwe siri baina yangu mimi na wewe, Sikukubishia japo mwanzoni  nilikukatalia kwa sababu najijua kifua cha kuficha siri sina.., Ila nikuahidi sitadiriki kuitoa popote na hata waliotuhisi tulikuwa tunawakatalia, iwe faragha au mbele ya hadhara tulitamka sio kweli, hapana hakuna kitu kama hiko, hayo ndiiyo yalikuwa majibu yetu”.

”Sasa umeondoka bila kunipa ruhusa juu ya hili je, niendelee kuitunza hii siri na je anavyoendelea kukua akija kuuliza na nikamwambia mama alisema uwe siri atanielewa kweli? Wallah Moyo wangu unauma Martha, hukupaswa kuondoka wakati huu, mapema mno,.. Dah Nenda Martha mwingi wa furaha a ucheshi, hata mama kasema leo msibani, jana ulikuwa unatabasamu hadi ulipofumba macho”

Marehemu Martha amewahi kuhojiwa na Kipindi cha Refresh cha Wasafi TV ambapo alificha ukweli uliopo kati yake na Mbosso akidai kuwa wawili hao ni marafiki tuu ambao urafiki wao hauwezi kutenganishwa.

”Mimi na Mboso ni marafiki, urafiki wangu mimi na Mboso hauwezi ukisha maisha yote hata iweje, na urafiki wangu na Mbosso” alisema Martha.

Marais 10 Afrika washiriki mazishi ya Mugabe
Walimu 10 mbaroni kwa wizi wa mitihani