Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kitendo cha kuwapeleka Wabunge 19 ambao hawakutokana na maamuzi ya chama ni uvunjaji wa Katiba, maadili na ni uhuni ambao hauwezi kuvumiliwa na yeyote.

Mbowe ameyasema hayo hii leo Machi 8, 2023 katika Kongamano la Baraza la Wanawake wa CHADEMA – BAWACHA, lililofanyika Mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan akinyanyua Tuzo maalum ya Maridhiano iliyotolewa na Baraza la Wanawake la CHADEMA – BAWACHA, kwa kutambua mchango wake wa kusimamia na kutekeleza maridhiano baina ya Serikali na vyama vya siasa na ukuzaji wa amani nchini.

Amesema, “Taasisi kama Bunge ambayo inapaswa kutunga sheria lakini inashiriki katika haya, pamoja na kuwa Spika anafahamu hakuna zuio lolote la wao kuwepo ndani ya Bunge lakini wameendelea kuwepo humo mpaka leo, ni uvunjaji wa Katiba, ni uvunjaji wa maadili na kitendo hicho ni uhuni.”

“Wale wanajiwakilisha wao wenyewe na familia zao hawamwakilishi mtu yeyote mule bungeni, Mheshimiwa Rais kwa heshima kubwa nakuomba uhurumie zile kodi za Wananchi ambazo mnawalipa wale Wabunge na hawamwakilishi mtu yeyote mule,” amesisitiza Freeman Mbowe.

Wafugaji kortini kwa kumteka na kumbaka mjamzito wa miezi nane
Mlipuko wauwa 18 katikati ya jiji, Fire wasitisha uokoaji kisa giza