Mbunge mmoja nchini Kuwait aliyetajwa kwa jina la Nabil Al-Fadl ameanguka ghafla na kupoteza maisha wakati kikao cha bunge kikiendelea.

Al-Fadl mwenye umri wa miaka 56 alionekana kwenye vipande vya video vilivyosambaa kwenye mitandao ya kijamii vikionesha akianguka kutoka kwenye kiti chake na kuanza kupewa huduma ya kwanza na waziri wa afya wa nchi hiyo, Dk. Ali Al Obaid hadi pale madaktari walipowasili lakini walishindwa kuokoa maisha yake.

Mbunge huyo alikuwa mwandishi wa habari machachari ambaye mara kadhaa aliwakosoa vikali wabunge wenzake na hata kuwakashfu.  Alikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wanamsapoti kutokana na misimamo yake ya kuikosoa serikali.

Alifahamika zaidi kwa kuwapinga vikali waasi wa kiislamu na kuwakaripia mara kadhaa alipopewa nafasi ya kuchangia bungeni na hata anapoandika kwenye gazeti lake.

Magufuli Amfyeka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Avunja Bodi Mbili
Waislam watoa maisha yao kuwalinda Wakristo dhidi ya Al-shabaab