Waislam waliokuwa wakisafiri katika basi moja na wakristo nchini Kenya wameripotiwa kujitoa maisha yao na kuwalinda wakristo baada ya kundi la Al Shabaab kuliteka basi hilo .

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia BBC kuwa wanamgambo wa Al-Shabaab waliliteka basi hilo lililokuwa likisafiri kutoka jijini Nairobi kuelekea Mandera Kaskazini mwa Kenya na kuwataka abiria kutengana katika makundi mawili, kwa maana ya waislamu na wasio waislamu.

Basi

Shuhuda huyo ameeleza kuwa waislamu walikataa kujitenga na wakristo licha ya kuelewa kuwa endapo wangejitenga wangeponya roho zao na wasiokuwa waislamu ndio pekee ambao wangeuawa.

Abiria walikaa pamoja bila kutengana na kuwaeleza wanamgambo hao wa Al-Shabaab kuwa hawako tayari kutengana na kwamba  ni bora wauawe wakiwa pamoja.

Katika tukio hilo, watu wawili waliripotiwa kuuawa na wengine watatu walijeruhiwa.

Mbunge afariki ghafla kwenye kikao cha bunge
Sherehe za Kumuombea Lowassa Uvumilivu, Hekima Nusura Zivunjike