Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kwa kutoa kifaa cha  kupima  Malaria kwa wananchi wa Kijiji cha Mtamaa kwa kuwapatia Mashine ya  (Binocular Microscope) Mega 7.

Sima amekabidhi mashine hiyo kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana

Amesema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na  maendeleo na kuwapa  haki usawa  raia wa Tanzania.

Kuhusu kero ya Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo ametoa ahadi mpaka kufikia  mwezi wa Nne mwakani maji yatakuwa yameanza kupatikana ili kumaliza tatizo hilo  kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.

Naye Mganga Mkuu wa zahanati ya Mtamaa  Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.

Unyama: mwanamke amuua mjamzito kwa kumpasua tumbo kwa kisu na kuiba mtoto
Madereva wa vigogo walia na agizo la JPM kurejesha fedha za Mwenge, 'hatuna kitu’