Wiki hii ilikuwa wiki ambayo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza mengi yaliyoteka vichwa vya habari.

Kati ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na uamuzi wa Rais John Magufuli  kuwasimamisha na kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa umma.

Membe ambaye aliwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, amekaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa ni rahisi kwa rais Magufuli kufanya hivyo kwa sababu watu anaowasimamisha hakuwateua yeye kwa sababu hawafahamu.

“Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini sio rahisi kumshughulikia unayemfahamu. Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” Membe alisema.

Vijana wa CCM wamvaa Membe, wamtaka amuache Magufuli
Mrembo wa UDSM aliyedaiwa kuwa Msukule uliokutwa shimoni anena kwa uchungu