Licha ya waziri wa uchukuzi wa Kenya, Kipchumba Murkomen kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya marubani, hali ya sintofahamu bado imeendelea katika safari za anga kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, baada ya hii leo Oktba 7, 2022 mgomo wa Marubani umeingia siku ya tatu.

Mgomo huo ulioanza Novemba 4, 2022 unatokana na madai ya Marubani ya kutaka nyongeza ya mishahara na marupurupu, huku hali hiyo ikiathiri wasafiri na bidhaa ambazo na hadi kufikia sasa jumla ya wasafiri 12000 waliokuwa wamelipa nauli wameathiriwa na mgomo huo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la Ndege nchini Kenya, Allan Kilavuka amewaonya marubani hao wanaogoma Kilavuka ameongeza kusema kuwa shirika hilo lilikuwa limepiga hatua tangu janga la Covid, lakini sasa mgomo huo unaathiri juhudi zilizokuwa zimefanywa. Amesisitiza kuwa mgomo huo ni haramu na unajiri wakati mbaya.

Chama cha marubani cha shirika hilo hakijaelezea mgomo huo utakamilika lini ingawa kimesema kuwa marubani wake watarejea kazini pindi tu mfuko wa malipo yao utakaporejeshwa pamoja na nyongeza ya mishahara.

Charles Lukula: Wakushukuriwa ni MUNGU
Simba Queens yalamba milioni 565.4