Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amewataka watumishi Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuongeza bidii ya uzalishaji na kuwa wabunifu katika kutafuta masoko zaidi nchini.

Ameyasema hayo alipofanya ziara Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili kukagua shughuli za uendeshaji wa kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali jijini Dodoma.

Amewasisitiza watumishi wa ofisi hiyo kuwa wabunifu kwa kutumia vifaa walivyo navyo ili kuongeza uzalishaji na kutafuta masoko zaidi nchini yatakayowasaidia kupata mapato zaidi ya kuendeshea shughuli za kiwanda hicho.

“Ni vyema mkatumia fursa ya taasisi na mashirika yaliyopo nchini kutafuta masoko ya kutengeneza majalada yao. Mfano tunao mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao utahitaji kutoa majalada mengi kwa ajili ya kuelimisha umma juu ya majukumu yao. hivyo ni vyema mkawa wabunifu kwa kuongeza bidii katika kutafuta masoko zaidi kwenye Wizara mbalimbali, Taasisi na Makampuni yaliyopo nchini.” amesema Mhagama

Hata hivyo, kwa upande wake Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Hyacinth Komba amesema kuwa watafuata maagizo ya waziri kwa kuboresha shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho na kuahidi kutekeleza majukumu yao.

 

Kangi Lugola achukua maamuzi magumu baada ya ajali ya Kigwangallah
Video: Mwisho wa vishindo vya Makonda, Waliochota Nida waanza kuzitema