Mlinzi anayelinda jeneza la Hayati Malkia Elizabeth II, ameanguka ghafla wakati wa maandalizi ya kuagwa kwa mwili wa Kiongozi huyo aliyeitawala Uingereza kwa muda mrefu (miaka 70), kwenye ukumbi wa Westminster Hall jijini London.

Tukio hilo, limetokea wakati raia wa Uingereza wakiendelea na zoezi la kuaga mwili wa Malkia huyo aliyefariki hivi karibuni, ambapo chanzo cha kuanguka kwa mlinzi huyo hakikuweza kufahamika mara moja.

Picha ikionesha mlinzi huyo alivyokuwa akianguka. Picha na ITV News.

Mara baada ya kuanguka kwa mlinzi huyo, Televisheni ambayo ilikuwa ikirusha matangazo hayo mubashara ilisitisha matangazo wakati mlinzi huyo akipatiwa matibabu ya dharura.

Jeneza la Hayati Malkia Elizabeth II, linalindwa kikosi maalum kinachofahamika kama Sovereign’s Bodyguard.

TPLB yasogeza mbele ratiba Ligi Kuu
Farouk Shikalo akubali lawama za mashabiki