Takriban watu 18 wamefariki dunia huko Bangladesh na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa mlipuko kwenye jengo moja lililo na mkusanyiko wa watu wengi kibiashara kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka.
Tukio hili linafanya jumla ya milipuko kufikia mitatu baada ya ile miwili ya awali, na kufanya jumla ya vifo vilivyotokana na milipuko yote mitatu kufikia watu 28, huku Mkuu wa Zimamoto jijini Dhaka, Dinmoni Sharma akisema shughuli za uokozi silisitishwa kutokana na giza.
Polisi nchini humo, wanasema mlipuko huo wa Jumanne Machi 7, 2023 umetokea kwenye kitongoji cha Siddik Bazar majira ya saa za jioni wakati wa wa uwepo wa msongamano mkubwa wa watu walikuwa wakipata mahitaji binafsi.
Takriban watu 140 wamelazwa kwenye hospitali ya dharura ya Medical College mjini Dhaka, kulingana na inspekta wa polisi wa kituo cha polisi cha hospitali hiyo, Bacchu Mia,wakati akizungumza na VOA, kuhusu watu waliolazwa kwenye hospitali hiyo.