Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, (WHO), limetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa ndui ya nyani au monkeypox Duniani ni tishio kwa afya ya umma.

Tangazo hilo, limetolewa hii leo Julai 23, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi baada ya kikao cha pili cha Kamati ya Kimataifa ya dharura za kiafya ya WHO kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa ndui ya nyani au Monkeypox.

Dkt. Tedros amesema, ingawa wajumbe wa kamati hawakufikia muafaka kuhusu ndui ya nyani kama ni tishio au la kwa mujibu wa vigezo vya kutoa tamko hilo, ametangaza kuwa mlipuko ni tishio na umeenea zaidi Ulaya.

Kwa mujibu wa Dkt. Tedros, mlipuko umeendelea kukua na hadi sasa kuna waonjwa zaidi ya 16,000 kutoka nchi 45 Duniani na vifo  vya watu watano vimeripotiwa.

Amesema, kilichobainika ni kwamba ugonjwa huo unasambaa zaidi miongoni mwa wanaume mashoga na wenye wapenzi zaidi ya mmoja na hivyo ni vyema kuchukua hatua kujikinga na iwapo hatua zitachukuliwa, ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa na mlipuko kudhibitiwa.

Tabora ‘wadeka’ usafiri huduma za TANESCO
Wamarekani wamiminika kutalii Tanzania