Waziri wa Nishati, January Makamba amezindua huduma ya usafiri wa Bajaji na Pikipiki zitakazowasaidia wananchi kupata huduma za TANESCO saa 24 kwa urahisi na haraka.

Uzinduzi wa usafiri huo, umefanyika Mkoani Tabora na ambapo pia anatarajia kuvifikia Vijiji mbalimbali vya Mkoa huo ikiwa sehemu ya Ziara yake ya siku 21.

Mara baada ya kufika Mkoa wa Tabora, Waziri Makamba amezindua matumizi ya Pikipiki za magurudumu mawili (Bodaboda), na Pikipiki za magurudumu matatu (Bajaji), ili ziwasaidie wananchi kufikiwa kwa urahisi pale wanapopata matatizo ya Umeme kwa saa 24.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akiwa na mfanyakazi waShirika Umeme nchini TANESCO, wakati wa uzinduzi wa huduma ya usafiri wa Bajaj na Pikipiki za kuwahudumia wananchi Mkoani Tabora.

Ziara ya Makamba, ni muendelezo wa kuwasaidia Wananchi wa chini kupata huduma ya Tanesco kwa urahisi kupitia mfumo wa viunga (Clusters), na idadi ya Bajaj zilizozinduliwa ni saba na Pikipiki kumi.

Serikali yawaasa Vijana kuthamini vipaji
‘Monkeypox’ tishio jipya afya Duniani