Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka watendaji wa Wizara ya Afya kuhakikisha Hospitali ya Mwera Pongwe inajengewa uzio ili kukinga maji yasiingie ndani mvua zinaponyesha.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizindua jiwe la msingi la Hospitali ya ya Mwera Pongwe.

Dkt. Mwinyi, ameyasema hayo hii leo Julai 23, 2022 wakati akikagua na kuweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo katika mwendelezo wa ziara yake iliyoanza Julai 16, 2022 ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoa wa Kusini Unguja.

Akiwa katika eneo hilo, pia Rais Mwinyi amewakumbusha Wananchi juu ya zoezi la kuhesabiwa siku ya Sensa tarehe Agosti 23, 2022 na kuwataka kudai risiti za kielektroniki pindi wanaponunua bidhaa.

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipewa maelekezo wakati wa ukaguzi wa jengo la Hospitali ya Mwera Pongwe.

Wamarekani wamiminika kutalii Tanzania
Zanzibar kuwa na uchaguzi wa kidemokrasia