Peter Msechu ameeleza mtazamo wake kuhusu msanii kupata au kutopata tuzo kunavyoweza kuchangia kumfikisha mbele zaidi msanii na kupima uwezo wake au la, ambapo amedai kuwa tuzo sio chanzo cha mafanikio makubwa ya msanii.

Msechu anaamini kuwa kupata tuzo ni sehemu ya pongezi tu ya kile ulichokifanya katika muziki wako kwa muda mrefu na kuonesha kuwa ‘umefika mbali’ lakini sio chanzo cha kukufikisha mbali.

“Sioni kama tuzo inaweza kukufanya wewe kufika mbali, kwa sababu umeipata baada ya wewe kufika mbali. Kinachoanza ni wewe kufika mbali na sio tuzo. Kwa hiyo jitihada ndizo zinakufanya wewe kufika mbali ndio unapata tuzo,”Msechu aliiambia East Africa Radio.

Alisema kuwa tuzo sio chanzo cha mafanikio ya muziki kwa kuwa haimpeleki msanii studio wala kumuandikia nyimbo zinazomfanya apate mafanikio hivyo kwake kupata au kukosa tuzo sio kipimo cha kufanikiwa au kushindwa kufanikiwa kwa msanii.

“Lakini mimi nafikiri kwamba tuzo ni heshima tu unayoipata baada ya kufika mbali. Sio kitu kizuri kusema umepata tuzo kwa hiyo wewe unaweza na wengine hawawezi kwa sababu mpaka unapata tuzo na mwingine amekosa tuzo, ni kwa sababu yule mwenzako alikuwepo kwenye kinyang’anyiro akakosa na wewe ukapata.”

Video: Angalia Interview ya ‘kibabe’ ya Ruby kwenye The Playlist ya Times Fm
Dkt. Bilal: Abiria ‘Kuchimba Dawa’ Porini Sasa Basi