Serikali imeipongeza Kampuni ya Benchmark kwa kutekeleza maelekezo yake kuhusu malipo ya mshindi wa BSS 2019 Meshack Fukuta kwa kumlipa sehemu ya fedha anazodai na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Sanaa Juliana Shonza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Mkurugenzi wa Benchmark Madam Rita chini ya usimamizi wa Basata amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni tano.

“Ili kuepuka kujitokeza kwa mazingira kama haya katika mashindano yajayo, Serikali itahakikisha utaratibu wa waandaji wa mashindano kukabidhi zawadi husika kwa BASATA kabla ya fainali ya Mashindano unatekelezwa”.amesema Naibu waziri Shonza .

Hata hivyo Shonza ametoa wito kwa Benchmark na Wadau wengine wanaoendesha mashindano mbalimbali ya vipaji kuzingatia kuweka zawadi wanazoweza kuzimudu kulingana na maandalizi yao ili kuepusha usumbufu usio wa lazima.

Mchezaji wa Arsenal yu mahututi
Mwamnyeto kubaki Coastal Union

Comments

comments