Kampuni ya Mini Bakeries LTD ya nchini Kenya imeahidi kumlipa fidia mteja aliyelalamika kupitia mtandao wa twitter kwamba alinunua mkate na kukuta kuanzia kipande cha kwanza hadi cha mwisho vina tobo katikati.

Kampuni hiyo ambayo inazalisha mikate ya Supa Loaf, licha ya kumuomba msamaha mteja wake huyo aliyedai kuwa ni mtumiaji wa mkate wa muda mrefu lakini bado haijabainisha itamfidia nini na kwa kiasi gani.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Supa Loaf wamendika hivi, “Habari Kellyinyani tumeiona tweet yako, tunaomba radhi pia tunaomba utuandikie anwani ya makazi yako na mawasiliano yako kupitia DM ili tuweze kukulipa fidia”.

Vipi ndugu msomaji, umeshawahi kuuziwa mkate au maandazi yenye tobo? Yapi maoni yako kwa mambo kama haya?

Wachezaji Young Africans wapumzishwa
Popat: Simba, Young Africans mnajisumbua