Uongozi wa Azam FC umeendelea kusisitiza suala la kufanya kazi na mshambuliaji wao kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube, licha ya kushamiri kwa tetesi za kuwaniwa na klabu za Simba SC na Young Africans.

Dube ambaye kwa sasa anaongoza kwenye orodha ya upachikaji mabao katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amekua akiwindwa vikali na klabu hizo nguli katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2020/21.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesisitiza kwamba hawana ofa yoyote na wala hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo.

“Kila siku watu wanasema kwamba Azam tunafeli wapi, sasa hivi tunajenga timu halafu tumuuze mchezaji ambaye anafanya vizuri, sisi wenyewe tunataka tuwe kama wao (Simba) sio kila siku tunaanza moja.”

“Dube bado ana mkataba na sisi hilo pia Simba wanalifahamu kabisa, tena sio mkataba mfupi kwetu.”

Mteja aliyeuziwa mkate wenye tobo kulipwa fidia
Kinyang'anyiro Miss Kagera chashika kasi