Mchakato wa kumpata mrembo atakayewakilisha Mkoa wa Kagera katika Shindano la Miss Tanzania 2021, umeanza kushika kasi katika mkoani humo, baada ya kamati ya maandalizi kwa kushirikiana na waandaaji kutambulisha rasmi zawadi ya mshindi wa taji hilo.

Akitambulisha zawadi hiyo mratibu wa Shindano la Miss Kagera 2021, Regina Zachwa kutoka Zachwa Investment amesema mwaka huu wao kama waandaaji waliopewa dhamana hiyo, kwa kushirikiana na Serengeti Breweries Ltd pamoja na wadau wengine wameamua kuandaa zawadi ya gari aina ya Rectus lenye thamani ya Shilingi Milioni 18 ambayo atapewa mshindi wa kwanza.

“Mara hii Miss Kagera itakuwa Kivingine na kubwa zaidi, ukizingatia Ukubwa wa zawadi ya Mshindi, lakini pia wapo Baadhi ya waheshimiwa wakiwemo Wabunge ambao wameamua kussuport Jambo Hili, hivyo tunategemea pia ushindani utakuwa Mkubwa Sana,” amesema Regina.

Zawadi hiyo ya Gari imezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro katika Viwanja vya Makao Makuu ya Redio Kasibante FM inayomilikiwa na Zachwa Investment, ambaye kwa Upande wake amesema Shindano hilo litautangaza Mkoa wa Kagera katika nyanja tofauti zikiwemo za kiuchumi na kiutamaduni, na kuwataka wasichana kujitokeza kushiriki katika mchakato huo.

Kamati hiyo ya Maandalizi ya Shindano la Miss Kagera imeweka wazi ratiba ya shindano hilo kwa Wilaya za Mkoa wa Kagera ambapo Mei 28 – 29 shindano litaanzia Biharamulo na Ngara na Juni itakuwa zamu ya Muleba na Missenyi, Julai zamu ya Karagwe na Kyerwa na kisha kilele cha shindano kufanykka Agosti 8, 2021 Mamispaa ya Bukoba.

Popat: Simba, Young Africans mnajisumbua
RC Dar kuwarejesha ombaomba makwao