Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla amesema kuwa Ofisi yake itaanza kushugulika na ombaomba waliozagaa katikati ya jiji kuanzia mwezi Juni mwaka huu kwa kuanza kuandikisha majina yao na vijiji walivyotoka lengo likiwa ni kuwarudisha makwao.

RC Makalla amewaagiza Wakuu wa Willlaya na wakurugenzi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo kikamilifu.

RC ameyasema hayo leo Mei 27, 2021 katika kikao na Asasi za kirai kinachohusu ni namna gani serikali inaweza kutatua swala la ukatili wa kijinsia.

Hata hivyo RC amewahasa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwatafuta makawakala wanaowatumia ombaomba hao kama kitega uchumi na kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya sheria

Sambamba na hayo yote RC Makalla amesema kuanzia sasa ofisi yake iko tayari kutoa nauli kwa ombaomba yoyote ambaye yuko tayari kurudi nyumbani bila shuruti ya serikali

Kinyang'anyiro Miss Kagera chashika kasi
Waziri Nchemba ashtukia njama tenda za Serikali, PPRA yaokoa Sh.30 bilioni