Mara nyingi amuzi hilo gumu huchukuliwa na watu wazima baada ya kukosa uelekeo au kukata tamaa katika maisha , lakini karne hii tunaona hata watoto wa dogo tena wa shule ya msingi kuchukua uamuzi huo.

Ni mwanafunzi wa darasa la tano  katika shule ya msingi Kizota Manispaa ya Dodoma, Yassin Abdallah amejinyonga kwa kutumia shuka bafuni baada ya kupata matokeo mabaya ya mitihani yake ya mwisho wa mwaka.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Ernest Kimola, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo.

Mtoto huyo katika matokeo yake ya mwisho alishika nafasi ya 128 kati ya wanafunzi 132, hali ambayo inadaiwa ilimshtua na kuamua kujinyonga.

Diwani Jamal alitoa rai kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuepuka kutoa vitisho ambavyo vitawasababisha wachukue maamuzi magumu.

 

Video: Dangote aja kushitaki kwa Rais Magufuli, Ukawa CCM kutikisa majukwaa kwa siku 30...
Mpina: Serikali ya awamu ya tano inaongozwa na nguvu za mungu