Muonekano wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa serikali ya awamu ya tano, Dkt. John Magufuli kuliondoa hofu za baadhi ya watanzania ambao hushindwa kuamini kwa maelezo hadi pale macho yao yatakaposhuhudia.

Mkapa alipata mapokezi ya hali ya juu ya shangwe za watanzania wengi waliohudhuria sherehe hizo baada ya kutajwa na kumshudia akiingia uwanjani akiwa buheri wa afya, mkakamavu kama kawaida yake na mwenye tabasamu lisiloficha furaha yake kutoka moyoni.

Shangwe hizo za maelfu ya wahudhuriaji zilitokana na taarifa zilizokuwa zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais huyo wa awamu ya tatu alifariki.

Hata hivyo, tayari taarifa hizo zilikuwa zimekanushwa vikali na Idara ya Habari Maelezo ambayo ilieleza kuwa ni buheri wa afya.

Mkapa ni mmoja kati ya watu waliokuwa na furaha zaidi kwani ndiye aliyeanza kumuamini Dkt. Magufuli na kumpa nafasi ya Naibu Waziri wakati wa utawala wake ambapo aliitumia vizuri nafasi hiyo na kupata sifa za kutosha.

Sifa hizo zilionekana wazi kwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliyeamua kumpa nafasi ya Uwaziri Kamili, nafasi ambayo ilimfanya ang’are zaidi kiutendaji na sifa zake kuwafikia wananchi wengi zaidi ambao mwaka huu wamezitumia kumpa kura za kutosha kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano.

Urusi yapinga Ripoti ya Marekani kuanguka ndege ya Nchi hiyo, Putin Afanya Maamuzi Magumu
Ronaldo: Mimi Ndiye Bora Duniani