Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema bado anaamini yeye ni bora katika mchezo wa soka kutokana na mambo makubwa anayoendelea kuyafanya anapokua ndani na nje ya uwanja.

Ronaldo ametangaza tambo hizo, alipokua akifanyiwa mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha shirika la utangazai la Uingereza BBC, usiku wa kuamkia hii leo.

Ronaldo, amesema kuendelea kuwepo katika historia ya soka kunampa faraja na kuamini jambo hilo linatosha kumpa imani anatosha kuwa bora duniani kote.

Amesema ni vigumu kwa mchezaji yoyote kuingia katika historia ya soka duniani, lakini kwake imekua hivyo kutokana na mazuri ambayo amekua akiyaonyesha uwanjani hadi kufikia hatua kutajwa kuwa mchezaji bora wa dunia mara tatu.

Kauli ya Ronaldo imetafsiriwa kama kijembe kwa mpinzani wake wa karibu Lionel Messi ambaye kwa mwaka huu wapo kwenye kapu moja la kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambapo hafla yake imepangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2016 mjini Zurich nchini Uswiz.

Ronaldo mpaka sasa amekuwa mchezaji wa kipekee katika ramani ya soka, kutoka na rekodi mbali mbali alizojiwekea huku akiwa mfungaji bora wa muda wote katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kufuatia mabao 82 aliyoyafunga.

Muonekano Wa Mkapa Ulivyosawazisha Mambo
Ujumbe wa Rais Magufuli kwa Lowassa na Wenzake