Rais wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewapa ujumbe muhimu waliokuwa washindani wake wakuu kwenye mbio za uchaguzi wa uliofanyika mwezi Oktoba, akiwemo aliyekuwa mshindani wake mkuu kupitia Chadema akiungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa.

Kupitia hotuba fupi kwa wananchi wa Tanzania na wageni mbalimbali mashuhuri waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake, Rais Magufuli aliwataka washindani wake hao kuungana katika safari mpya ya kulijenga taifa.

“Ninyi mlikuwa washindani wangu na sio wapinzani wangu maana sote tulikuwa na lengo la kujenga nchi moja. Ninawashukuru kwa changamoto mlizonipa,” alisema.

Rasi Magufuli aliwashukuru pia washindani hao na kueleza kuwa ushindani wao umemfunza mengi mazuri atakayoyafanyia kazi katika kipindi cha uongozi wake.

“Nimejifunza mengi kutoka kwenu. Lakini nimejifunza mengi mema ambayo nitayafanyia kazi ili kujenga taifa bora.”

Lowassa Peoples Power

Pia, Rais Magufuli alikuwa na ujumbe wa jumla kwa vyama vya siasa na wafuasi wake ambapo aliwataka kuweka kando tofauti zao na kuungana kulijenga taifa moja akisema kuwa Tanzania ni kubwa zaidi ya vyama vya siasa.

Baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi ya urais walishiriki katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Dkt. Magufuli huku mshindani wake mkuu, Edward Lowassa ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani akikosekana katika sherehe hizo.

Lowassa alipinga utaratibu wa ukusanyaji wa matokeo na utangazaji wa matokeo hayo uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo aliwasilisha hati ya pingamizi kutaka zoezi la utangazaji wa matokeo hayo kusitishwa kwa madai kuwa matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na Tume hiyo yalitofautiana na yale yaliyokuwa katika vituo vya kupigia kura.

Hata hivyo, siku chache baadae, Lowassa alionekana katika hafla ya kuiaga timu yake ya kampeni na kuwataka kutokata tama kwa kuwa safari ndio kwanza imeanza na kwamba awamu nyingine inakuja.

Ronaldo: Mimi Ndiye Bora Duniani
Ziara ya ghafla ya Rais Magufuli yaibua haya Wizara ya Fedha