Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameanza rasmi kuifanyia kazi kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’ambapo leo amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ilianzia Ikulu ambapo Rais Magufuli aliondoka kwa mwendo wa miguu na mlinzi wake bila kuwapa taarifa wafanyakazi wake wengine na kuelekea katika ofisi za Wizara ya Fedha zilizoko umbali usiozidi mita 100.

Rais Magufuli Wizara ya Fedha

Picha za video zilizotumwa katika tukio hilo, zinamuonesha Rais Magufuli akiwa ndani ya ofsi za Wizara hiyo na kubaini wafanyakazi wengi ambao hawakuwa ofisini muda huo huku kiongozi wao akidai walienda kunywa chai.

Mtindo huu wa kufanya ziara za kushtukiza ulikuwa ukitumiwa pia na mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete hasa wakati wa mwanzo wa uongozi wake mwaka 2005.

Kikwete alifanya zira za ghafla katika baadhi ya masoko jijini Dar es Salaam na kuulizia bei za bidhaa kama mwananchi wa kawaida. Pia, alitembelea baadhi ya hospitali na kujionea uhalisia wa huduma za kiafya bila kufanyika kwa maandalizi ya kumpokea.

 

Ujumbe wa Rais Magufuli kwa Lowassa na Wenzake
Ubelgiji Yaandika Historia Kwa Mara Ya Kwanza