Timu ya taifa ya Ubelgiji, imeiwezesha nchi hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa soka duniani vya mwezi Novemba.

Ubelgiji wamekamata nafasi hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza katika histoaria ya soka duniani, kufuatia mazuri waliyoyaonyesha katika kipindi cha hivi karibuni.

Mwezi uliopita, Ubelgiji ilikua inashika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora wa soka duniania mbavyo hutolewa na FIFA, kwa kutanguliwa na nchi za Argentina na Ujerumani.

Sifa kubwa iliyoibeba nchi hiyo, ni harakati za matokeo mazuri yaliyokua yakipatikana wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 ambazo zitaunguruma nchini Ufaransa.

Timu ya taifa ya Chile nayo imeliwezesha taifa hilo kupanda na kufika katika nafasi ya tano, ikitokea nafasi ya tisa ikiwa ni kiwango kikubwa kufikiwa katika historia ya soka duniani.

Kumi bora ya viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Novemba ni kama ifuatavyo.

1 (3) Belgium 2 (2) Germany 3 (1) Argentina 4 (4) Portugal 5 (9) Chile 6 (6) Spain 7 (5) Colombia 8 (7) Brazil 9 (10) England 10 (11) Austria.

Muhimu: Namba zilizowekwa kwenye mabano ni nafasi za mwezi uliopita kwa nchi husika.

Ziara ya ghafla ya Rais Magufuli yaibua haya Wizara ya Fedha
Mourinho Afungiwa Milango Ya Uwanja