Chama cha soka nchini Engalnd FA, kimeiweka kapuni rufaa ya meneja wa klabu bingwa nchini humo, Chelsea, Jose Mourinho.

Mourinho alikata rufaa ya kupinga adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja na kutozwa faini ya paund 50,000, kufuatia kauli ya kidhalili ambayo aliitoa mbele ya waandishi wa habari dhidi ya muamuzi Robert Madley, aliyechezesha mchezo kati ya Chelsea na Southampton.

Mourinho alieleza bila uwoga juu ya muamuzi huyo, kwa kusema liwabeba wazi wazi wapinznai wao ambao waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja kwenye uwanja wa Stamford Bridge mwezi uliopita.

Kukataliwa kwa adhabu hiyo, kunadhihirisha Mourinho hatoruhusiwa kuingia uwanjani hapo kesho wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England ambapo kikosi cha Chelsea kitakua ugenini kikipambana na Stoke city.

Ubelgiji Yaandika Historia Kwa Mara Ya Kwanza
Tanzania, Kenya, Uganda Zapanda Viwango Vya Soka