Nchi za Kenya na Tanzania zimepanda kwenye orodha mpya ya viwango vya soka duniani ambayo hutolewa kila mwezi na shirikisho la soka duniani, FIFA.

Kenya imepanda kwa nafasi sita ikitokea namba 131 hadi 125, huku Tanzania ikapanda kwa nafasi moja kutoka namba 134 hadi 135.

Tanzania imebebwa na sifa ya kufanya vyema katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, kwa kuifunga timu ya taifa ya Malawi jumla ya mabao mawili kwa moja.

Katika orodha ya viwango vya soka duniani ya mwezi Novemba, Malawi inaonekana katika nafasi ya 97 kwenye orodha hiyo.

Ivory Coast ndiyo inayoongoza barani Afrika lakini kwa upande wa viwango vya dunia ipo katika nafasi ya 22, ikifuatwa na Algeria inayoshika nafasi ya 26 huku Ghana ikishika namba 30.

Uganda wanaendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika mashariki lakini kwa upande wa dunia wapo kwenye nafasi ya 68 baada ya kupanda nafasi saba.

Rwanda inashika namba 96 baada ya kushuka kwa nafasi tatu ili hali majirani zao Burundi wapo katika nafasi ya 107 kufuatia kupanda kwa nafasi sita.

Congo Brazzaville wanashika nafasi ya 52 duniani, wakifuatwa kwa karibu na DR Congo walio kwenye anfasi ya 55.

Sudan wameshuka hatua kwa nafasi 44 na sasa inakamata namba 128, na Ethiopia ipo kwenye nafasi ya 117 baada ya kuporomoka kwa nafasi sita.

Sudan Kusini waliocheza mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la dunia dhidi ya Mauritania, ambayo walitoka sare ya bao moja kwa moja  lakini wakabanjuliwa kwenye mchezo wa mkondo wa pili kwa kucharazwa mabao 4-0, wanashikilia nambari 134 baada ya kupanda nafasi 10.

Djibouti ndio wanaoshika mkia katika bara la Afrika wakiwa nambari 207, wakifuatiwa na Somalia nambari 203 na Eritrea 202.

Mourinho Afungiwa Milango Ya Uwanja
Dkt. Magufuli Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Tanzania, JK astaafu Rasmi