Kilio cha Wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakiitaka serikali mara kwa mara kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa ambayo imekuwa mwiba kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18.

Baada ya kusikia kilio hicho serikali imedhamiria  kufanya marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kuhakikisha marekebisho ya kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa, kinachoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa vinafanyiwa marekebisho kwa kuwasilisha muswada Bungeni kabla ya mwaka kuisha.

unnamed (10)
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipokua akiongea kwenye ujumbe wa wanaharakati wa masuala ya maendeleo ya jinsia na watoto walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni.

Waziri Ummy  alisema jitihada hizo za kufanya mabadiliko ya sheria zitahusisha pia sheria ya Mirathi inayomnyima mtoto wa kike na wanawake kurithi mali

Akizungmza kwa niaba ya wanaharakati katika ujumbe huo, mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Liliani Liundi alisema  ipo haja ya Serikali kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha sheria ya Ndoa kifungu cha 13 na 17 inafanyiwa marekebisho, kwakuwa inarudisha nyuma jitihada za kuleta usawa wa jinsia nchini.

Aidha, alieleza kuwa mabadiliko ya Sheria ya Elimu katika kifungu kinachokataza kuoa / kuoza mtoto wa shule ya Msingi na Sekondari ni jitihada inayohitaji kuungwa mkono.

“Ipo haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuwalinda watoto walio nje ya shule, kwakuwa mabadiliko haya ya sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la 11 yawewaacha nje pasipo ulinzi wa sheria watoto wengi walio nje ya shule”Alisema.

Kuhusu uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi, mhe Ummy alisema bado ni suala la kipaumbele kwa Serikali na hasa kwa kuwa Tanzania imekubali Itifaki ya SADC ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya kufikia 50/50 ifikapo mwaka 2030.

Ujumbe wa wanaharakati uliwasilisha maoni yao na changamoto mbalimbali zinazo ikabili nchi katika kuleta maendeleo ya mtoto na usawa wa jinsia nchini, ikiwa ni pamoja na suala la Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Nafasi ya uwakilishi wa mwanamke katika vyombo mbalimbali vya maamuzi. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bibi Lilian Liundi na Wanaharakati wa Shirika la LHRC, WAJIKI, TANZANIA Widows Association na shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAGIC).

Ukusanyaji ushuru wazua utata kampuni, watumishi Jiji
Picha: Diamond afanya mazungumzo haya na Waziri Mkuu nyumbani kwake