Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, jana alimkaribisha nyumbani kwake CEO wa WCB, Diamond Platinumz na kufanya nae mazungumzo yaliyolenga kukuza muziki wa Tanzania.

Diamond ambaye alifika nyumbani kwa Waziri Mkuu akiwa na meneja wake, Babu tale, amewaambia mashabiki wake kupitia Instagram kuwa walishauriana namna nzuri ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine kubwa ya soko la kimataifa.

“Muda mfupi uliopita Nyumbani kwa Mh Waziri mkuu kassim Majaliwa tulipokuwa tukizungumza nae mawili matatu Namna ya kuupeleka Soko la Muziki wa Tanzania katika Hatua nyingine kubwa itayofaidisha wanamuziki, Wadau na Taifa kwa Ujumla…. Hakika najivunia na kufarijika sana kupata Waziri Mkuu mkarimu na Serikali iliyo na nia na juhudi ya kusaidia Tasnia yetu ya Muziki na Sanaa kwa Ujumla,” ameandika kwenye Instagram.

Muswada wa Sheria ya Ndoa Kufika Bungeni Mwaka Huu
Maji 14 wanolewa kuwafunga mafisadi ndani ya miezi 9