Msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya amesema idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi huko Kalehe imeongezeka na kufikia watu 438 huku muujiza wa watoto wawili wachanga ukitokea baada ya kukutwa wakielewa juu ya maji wakiwa hai.
Muyaya ameyasema hayo wakati akiongea na vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, wiki moja baada ya kutokea mafuriko hayo makubwa, watoto wawili wachanga waliokolewa kimuujiza wakiwa hai, wakielea kwenye maji ya Ziwa Kivu.
Mashirika ya kiraia yanasikitishwa na kucheleweshwa kwa huduma za uokozi na ambazo hazina nguvu na kuzidiwa na uwezo na kwamba shughuli za uokozi zinaendelea katika maeneo yote yaliyoathiriwa.
Hata hivyo, serikali ya DRC imesema inadhibiti hali ya mambo na kuhakikisha juu ya usimamizi wa maafa hata kama hawawezi kuamua idadi kamili ya watu waliopotea ambayo mashirika ya kiraia yanakadiria kuwa elfu kadhaa.