Waziri Mhagama amesema Serikali imebadilisha muundo katika Sekretarieti za Mikoa na hivi sasa wanamtambua Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia utawala na rasilmali watu kama msimamizi wa maadili na haki za watumishi kwenye Halmashauri.

Waziri Mahagama ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambapo alizungumza na viongozi wa Mkoa, Wilaya na Watumishi wa Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma, akiwakumbusha watumishi hao wajibu wa kikazi.

Amesema, “Tumempa majukumu ya kusikiliza malalamiko na kero za watumishi, kuendesha mabaraza ya wafanyakazi lakini kubwa tumempa jukumu asimamie maadili na kuzuia mianya ya rushwa kwenye Halmashauri zetu.”

Akizungumzia suala la mishahara, Mhagama amesema, “kulikuwa na tatizo la watumishi kutolipwa malimbikizo ya mishahara (arrears) ambayo Mheshimiwa Rais aliamua yote yalipwe. “Kulikuwa na watumishi 113,964 ambao walikuwa wanadai arrears na tumetumia shilingi bilioni 196.68 kulipa hizo arrears.”

Wafunga maduka kushinikiza nafuu ukali wa maisha
Asakwa na Polisi kwa mauaji ya mkewe