Maafisa wa serikali ya Angola na raia wa kawaida wametoa heshima zao kwa Rais wa zamani Jose Eduardo Dos Santos, aliyefariki wiki iliyopita, huku ukiibuka mvutano wa eneo la kumuhifadhi kiongozi huyo.

Hata hivyo, mbali na sifa alizonazo Rais huyo wa zamani wa Angola aliyetawala taifa hilo la kusini mwa Afrika hadi 2017, mzozo kuhusu pahala pake pa kupumzika unaendelea.

Watoto wakubwa wa Dos Santos, wametaka uhakikisho wa ulinzi wa mwili na eneo la kufanya maziko nchini Uhispania, wakati mjane, Ana Paula dos Santos, na watoto wadogo wanataka mwili wake urejeshwe Angola.

Rais wa zamani wa Angola, Hayati Jose Eduardo Dos Santos.

Juhudi za kutaka Dos Santos kuzikwa nchini Uhispania, zinaongozwa na mmoja wa mabinti wa kiongozi huyo wa zamani, Tchize dos Santos, .

Tchize anasema, msimamo wake unataka kuzuia kifo cha babake kisitumike na Rais wa sasa Joao Lourenco, ambaye anafanya kampeni za kuchaguliwa tena Agosti 2022.

Inasemekana kuwa, Luanda alikodi kampuni ya mawakili kuwakilisha serikali katika vita hivyo vya kisheria.

Vyombo vya habari vya ndani nchini humo, vinasema Serikali ya Angola na familia ya marehemu Dos Santos, walijaribu kufikia makubaliano kuhusu mipango ya mazishi, lakini ilishindikana.

Sehemu mojawapo iliyoandaliwa nchini Angola kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni wanaofika kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hayati Jose Eduardo Dos Santos.

Mahakama ya Uhispania inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ulinzi wa mwili huo mwishoni mwa wiki hii.

Mmoja wa Viongozi wa Kitaifa nchini Angola akisaini kitabu katika kumkumbuka Rais wa zamaniwa nchi hiyo Hayati Jose Eduardo Dos Santos.

Ahmed Ally: Tutatambulisha wengine watatu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 14, 2022