Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa ameikimbia nchi kwa kutumia ndege ya jeshi kabla ya siku rasmi ya kujiuzulu ambayo ni leo jumatano july 13, 2022.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka vyomba vya Habari vya Kimataifa, zimesema kuwa Rais Gotabaya Rajapaksa amewasili nchini Maldives.

Rais Rajapaksa mwenye umri wa miaka 73, alitarajiwa kukabidhi madaraka baada ya yeye na Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe kukubali kuachia ngazi.

Mamia ya waandamanaji nchini Sri Lanka.

Kujing’atua kwa mwanasiasa huyo, kunatamatisha utawala wa ukoo wake ulioiongoza Sri Lanka kwa miongo kadhaa.

Wananchi wa Sri Lanka, wamesherehekea baada ya kupata habari juu ya kukimbia kwa rais wao, Rajapaksa ambaye analaumiwa kwa kusababisha mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Taarifa za kukimbia kwa Rais Rajapaksa akiwa na mkewe na walinzi wake, zimetolewa na Shirika la habari la AP.

Rais ateua mrithi wake, akimbia nchi
Samia aridhia msamaha wa riba wadaiwa sugu ardhi