Wananchi katika kijiji na kata ya Guta, wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya walimu katika kata hiyo, kwa kufanya ngono na wanafunzi na kuishi nao kinyumba kama wake zao.

Hatua hiyo ya kulaani imetokana na hivi karibuni kumkamata mwalimu wa shule ye Msingi Guta, akiishi na mwanafunzi wa shule hiyo kinyumba kama mkewe.

Wananchi wa kata hiyo wakiongozwa na diwani wao, Kigo Nyamhanga, jana waliwaambia waandishi wa habari kwa njia za simu za mkononi kuwa hivi karibuni katika kijiji cha Guta, walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo (jina linahifadhiwa) akiishi na mwanafunzi wa shule hiyo nyumbani kwake.

Walisema hivi karibuni saa za usiku walimkamata mwalimu huyo anayefundisha katika shule ya msingi Guta, akiwa na mwanafunzi mmoja wakiishi naye nyumbani kwake kama mke wake.

Kufuatia tukio hilo, diwani huyo alikemea tabia hiyo na kuwataka walimu katika kata hiyo, kuachana na tabia hiyo chafu, kwani wao wanapewa watoto kuwalea na kuwafundisha na siyo kuwafanyia ukatili huo wa kijinsia.

Aliongeza kamwe tabia hiyo katika kata yake, haiwezi kuvumiliwa ndani ya jamii na hata serikali kwa ujumla.

 

Tanzania yaibuka kidedea kwa kupata tuzo nyingi za Watsup TV Africa 2016
Video: Wananchi Ruangwa watakiwa kujenga vyoo, wapewa wiki mbili