Mwanasheria wa Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, Nduruma Majembe amesema bado wamedhamiria kwenda mbele kusaka haki, ili kumuwezesha mteja wake kucheza soka akiwa na amani ya moyo.

Fei ‘Toto’ ameingai kwenye Sakata zito na Uongozi wa Young Africans, baada ya kutangaza kusitisha mkataba mwishoni mwa mwaka 2022, lakini Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imepinga uamuzi huo na kumtaka kiungo huyo kurejea Jangwani, kwa kusisitiza Mkataba baina ya pande hizo mbili bado upo kisheria hadi mwaka 2024.

Mwanasheria Majembe amesema pamoja na maamuzi hayo ya Kamati ya ‘TFF’, bado mteja wake ameshikilia msimamo wa kutaka suala lake lipelekwe katika vyombo vya juu, akiamini ana haki ya kucheza soka lake tofauti na Young Africans.

Majembe amesema kwa sasa wanakamilisha taratibu za kwenda Mahakama ya Usulushishi wa Michezo Duniani ‘CAS’, huku wakidhamiria kuiomba FIFA kutoa ruhusa kwa Feisal kusajiliwa na Klabu nyingine ili kulinda kipaji chake.

“Mteja wangu Feisal hajakubaliana na maamuzi ya Kamati, hivyo tunajiandaa kwenda kukata rufaa ‘CAS’, huku akiendelea kufanya mazoezi binafsi, msimamo wake bado haujabadilika, hayupo tayari kurejea Young Africans,”

“Wakati tukisubiri majibu hao ‘CAS’, haraka tumepanga kuandika Barua FIFA ili kuomba mteja wangu aruhusiwe kusajiliwa na Klabu nyingine na sio Young Africans, hii ni kwa ajili ya kulinda kipaji chake.” amesema Majembe

Kocha Mbeya City: Tunaimudu Simba SC
Robertinho: Sikuwa na maana mbaya