Idara ya ujasusi ya Marekani imesema kuwa mtu aliyeonekana jana akipita karibu na Ikulu ya nchi hiyo akiwa na bunduki amesababisha kufungwa ghafla kwa vitu vyote kama hatua ya tahadhari.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa askari wa idara hiyo ya ujasusi alifanikiwa kumdhibiti mtu huyo aliyekuwa amejifunika sura kwa ‘mask’.

Mtu huyo ambaye jina lake bado halijawekwa wazi, alifikishwa katika kituo cha polisi baada ya mvutano kati yake na maafisa hao.

Anakabiliwa na mashtaka ya kubeba silaha ya moto bila kuwa na leseni, kugoma kukamatwa, kuvunja sheria huku akiwa ameficha sura yake kwa kitambaa maalum pamoja na makosa mengine ya sheria za usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa CBS News, Rais Barack Obama hakuwa Ikulu wakati huo kwani alikuwa Maryland.

Jokate aichambua show ya Ali Kiba Fiesta, “Hushindani na yeyote TZ”
Pacquiao amtwanga Vargas, aweka rekodi ya kipekee ya ubingwa wa dunia