Klabu ya Brighton & Hove Albion ya England imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Zambia Enock Mwepu kutoka klabu ya RB Salzburgy ya Austria.

Mwepu amesaini mkataba wa miaka minne na miamba hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini England.

Ni siku chache zilizopita tu nyota mwingine wa kimataifa wa Zambia alisaini mkataba wa kuitumikia Leicester City ya Uingereza akitokea hapohapo Salzburg,Patson Daka.

Kenneth Muguna kutua Jangwani
Kocha Matola aijibu KMC FC 'TUTAPAMBANA'