Kupitia mtandao wa Goal.com umeripoti kuwa klabu ya Young Africans ya Tanzania imekamilisha mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Gor Mahia ya Kenya, Kenneth Muguna.

Goal.com imeripoti taarifa hiyo huku ikikumbukwa mwanzoni mwa msimu huu, Muguna ambaye alikuwa nahodha wa Gor Mahia kabla ya kuvuliwa unahodha ambao alipewa Harun Shakava, alikuwa karibu kusaini Jangwani lakini dili hilo likashindikana.

Muguna amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Gor Mahia msimu huu na alikuwa katika kiwango kizuri mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili, Julai 04), waliposhinda Derby ya Mashemeji dhidi ya AFC Leopards ya Patrick Aussems (4-1) na kutwaa Kombe la FA.

Endapo taarifa za Muguna kutua Young Africans zitakua za kweli, atakua mchezaji wa pili wa Kimataifa kusajiliwa katika kipindi hiki, baada ya usajili wa Djuma Shaban kutoka AS Vita Club ya DR Congo.

Bumbuli: Wananchi vimbeni, "Simba haitufungi tena"
Mwepu kucheza England