Mfalme wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf amepanga kuingia katika siasa na kuachana na muziki.
Mzee Yusufu ameiambia East Africa Radio kuwa anatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge na kwamba endapo akiupata itambidi aache kabisa muziki.

“Kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nichague moja, itabidi kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja hivyo wapenzi wa muziki wangu lazima waelewe kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine ambazo ni nyingi na zinahitaji uwepo wangu,” alikiambia kipindi cha Tam Tam cha East Africa Radio.

Mzee Yuusuf anatarajia kuachia album mbili za mwisho kabla hajaacha muziki na kufanya mambo mengine ikiwa ni pamoja na kuisimamia bendi yake.

Huddah adai alikuwa ‘Kayai’ wa Mzee Ojwang!
Mastaa Wa Marekani Wamuimbia Tajiri Wa ‘Unga’ Aliyetoroka Jela, ‘El Chapo’, Sikiliza Hapa