Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amejiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Hayo yamethibitishwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kagaigai ambapo amekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa mbunge huyo.
Kagaigai amesema kuwa Nape ameandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo na tayari spika amempatia nakala ya barua hiyo.
”Ni kweli nimeiona barua aliyomwandikia Spika na mimi nimepata nakala yangu kwa hiyo ni kweli amejiuzulu labda awe na mawazo mengine, kama atabadiri ”, amesema Kagaigai.
Hata hivyo, Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo sasa ipo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe.