Katika nchi ya Amerika ya Kilatini, yenye vikundi vingi vya Kijambazi, makundi ya wizi, utesaji, utekaji na mauaji yanayotokana vikundi hivi, Nchi yenye Volkano na Matetemeko ya ardhi anaibuka Kijana Bishoo.
hapa kuna Kijana bishoo na Rais wa Taifa hilo, Nayib Bukele anayetokea katika familia ya Kitajiri yenye asili ya Kipalestina, waliohamia na kuishi nchini El Salvador, nchi ya hatari, huku akitokea kuipenda Siasa na kutamani kuingia kwenye medani hizi lakini baba yake anamsihi aachane nazo kabisa.
Baada ya kugombea Umeya, na kushinda kwa kishindo katika Mji mdogo wa Nuevo Cuscatlan ikabidi baba yake asiwe na hiyana sasa akubali tu kuwa Kijana na fundi wa Siasa, ikabidi ampe baraka za kuendelea na Siasa.
Kwa kipindi takribani cha miaka mitatu, akaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na kupata umaarufu mkubwa sana na hii ikapelekea kumpa nguvu ya kugombea katika Jiji kuu la nchi ya Jamhuri ya watu wa El Salvador, Jiji la San Salvador,
Akiwa Meya wa Jiji hili, alileta maendeleo katika Ujenzi wa miundombinu, aliboresha Elimu, Afya Teknolojia pamoja na masuala ya Usalama hata katika kupambana na makundi ya Ujambazi, akajitanabaisha katika kupinga Ufisadi na kuleta Uongozi mpya si kama uongozi uliozoeleka hapo zamani.
Alifanya vema sana, na akapata umaarufu mkubwa katika Jamhuri ya El Salvador na kupendwa zaidi, huku kukubalika kwake huku kukamletea matatizo, kwani Chama chake cha FMLN kikamtimua kikihofia harakati zake za kupambana na Ufisadi pamoja na kivuli chake.
Hatua hii ikampelekea kuanzisha Chama chake cha NI, na akaingia Ulingoni kugombea Urais sera yake kubwa ikiwa ni kupambana na rushwa, kuwahakikishia raia usalama dhidi ya makundi makubwa ya Kijambazi likiwemo kundi la Mara Salvatrucha 13 (MS13),
Matokeo ya Uchaguzi yakatangazwa, Hamadi, Malakaaaa! …. Nayib Bukele akatangazwa mshindi katika nafasi ya Urais akiwa na umri wa miaka 37, akitokea kwenye Chama chake hicho kipya, na kilichopenya kiurahisi kwenye ushindi huo.
Rais Nayib Bukele ni mwanasiasa maarufu zaidi Latin America ingawa wapo wanaoukosoa Uongozi wake hasa katika kupambana kwake na Majambazi, Rushwa na Ufisadi, na kituko kimoja kikubwa alichowahi kukifanya Nayib Bukele ni kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN General Assembly).
Rais huyu alitoa hotuba na kujipiga picha Kikongo wanasema (Kalanga Photo) ni mambo ya Ekotite haya kwa Kingoni tunasema Selfie na alipoulizwa ni kwanini amefanya hivyo akajibu kuwa, “picha hii ikienda Instagram itapeleka ujumbe kuliko hizi hotuba tunazotoa.”
Credit: Ibrahim Jeremiah.