Siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutakiwa kutimiza ahadi yake ya kuweka vifaa vya kupima wabunge kama wametumia kilevi ama dawa za kulevya kabla ya kuingia Ukumbi wa Bunge,  amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mtani wake, hivyo watu wasijali maneno yake.
Aidha, katika Mkutano wake uliofanyika juzi, Makonda alimuomba Spika Ndugai kuweka kipimo hicho ili kabla wabunge hawajasimama kuchangia hoja wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.
“Kaka yangu Ndugai alisema ana nia ya kuweka kifaa maalumu kuwapima wabunge kama wanatumia dawa za kulevya au la, hivyo atimize nia yake hiyo ili kama na huko wapo tuwanyofoe,” alisema Makonda.
Kwa upande wake Spika Ndugai, amesema kuwa Makonda ni mtani wake kwa kuwa yeye ni Mgogo na Makonda ni Msukuma hivyo huwa wanataniana na kuongeza kuwa mtu yeyote asijali kuhusu maneno hayo kwani alikuwa anamchapa kidogo tu.
Hata hivyo, wakati wa mkutano wa tatu wa Bunge la 11 Mei mwaka jana, Spika Ndugai alilieleza Bunge kuwa anafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa wabunge.

Trump aitaka Israel kusitisha ujenzi wa makazi eneo la West Bank
Wabunge Zanzibar wacharuka, watunga sheria kumdhibiti Maalim Seif