Rais wa Marekani, Donald Trump amemkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani, na kusema atafanya kazi kwa bidii kwa kile alichokiita makubaliano ya Amani kati ya Israel na Palestine.

Amesema pande zote mbili zinahitajika kuwa na makubaliano, na kwamba anataka Israel isitishe ujenzi wa makazi unaoendelea.

Kwa upande wake, Benjamin Netanyahu amesema Israel ni lazima ihakikishe kuwepo kwa usalama katika eneo la linalokaliwa na wapalestina la West Bank.

Amesema hivi sasa kuna fursa kubwa ya kuwepo kwa makubaliano ya amani kwa kushirikisha wajumbe wengine wa nchi za kiarabu.

Hata hivyo, Netanyahu amesema anaamini kwamba uongozi wa Donald Trump unatoa fursa ya kihistoria ya kubadilisha kile alichokiita kama kuwepo kwa wimbi la waislamu wenye msimamo mkali

Magazeti ya Tanzania leo Februari 16, 2017
Ndugai atema 'cheche' ajibu mapigo ya Makonda