Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kujipanga kutumia Nishati ya  Mkaa mbadala kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuilinda misitu isiharibiwe.

Waziri Ndumbaro ametoa wito huo wakati akizindua mkakati wa utekelezaji wa sera ya misitu ya (1998) na utiaji saini wa kanuni za uendelezaji wa Nishati ya Mkaa mbadala uliofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoani Ruvuma.

Aidha kusainiwa kwa kanuni hizo kutachagiza maendeleo ya Viwanda vinavyochakata mkaa huo, pia amesema watanzania hasa waishio mijini wakitumia mkaa mbadala basi misitu itaendelea kuwa salama na kuvifanya viumbe vinavyoishi kwenye misitu hiyo viendelee kuongezeka kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.

Hata hivyo Waziri Ndumbaro amesema kuwa hadi sasa nchini wafanyabiashara 19 wameanzisha viwanda vya kuchakatia Nishati ya mkaa mbadala hivyo kupitia kanuni zilizosainiwa zitawasaidia kupata uwezo wa masoko ndani na nje ya nchi hivyo kuifanya ajira iweze kuongezeka.

Kwa upande wake Kamishina wa Uhifadhi wa Wakala wa Huruma za Misitu (TFS),  Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa Mkaa Mbadala unapatikana kwa masalia ya miti na mabaki ya mimea mbalimbali ikiwemo mazao yanayolimwa na Wananchi.

Profesa Silayo amesema pia licha ya kulinda misitu lakini bado hata mwananchi ambaye ni mkulima atanufaika na mabaki ya mimea ya mazao yake kwa kuwa anaweza akayauza na kisha kumuingizia kipato cha fedha.

Meneja TTCL Kagera atumbuliwa
Makasha ya kusambaza Kondom yazinduliwa