Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa (NEC), Kailima Ramadhan amevitaka vyombo vya habari vya Tanzania viige mfano wa wenzao wa Kenya kwa kutumia muda mwingi kutoa elimu ya mpiga kura.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Mizani ya wiki kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha AZAM, ambapo amesema kuwa moja ya mambo aliyojifunza katika uchaguzi mkuu wa Kenya ni jinsi vyombo vya habari vilivyoshiriki katika uchaguzi huo na kuchangia watu wengi kujitokeza kupiga kura..

“Natamani nasisi vyombo vya hapa nyumbani viige wenzao wa Kenya ambao walitoa muda mwingi kwa kutoa elimu ya m piga kura,” amesema Kailima

Amesema kuwa baadhi ya mambo ambayo amejifunza kwa Tume Huru na Mipaka ya Kenya (IEBC) katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni ni usambazaji wa vifaa katika vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Aidha, Kailima ameongeza kuwa Kenya wana vituo vichache takribani 40,000 vya kupigia kura ukilinganisha na vya Tanzania ambako kuna vituo 65,000, lakini amesema walifanya vizuri kwenye kusambazavifaa.

Hata hivyo, Kuhusu kuruhusu wafungwa na Watanzania walioko nje kupiga kura, Ramadhan amesema kuwa kwa sasa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu jambo hilo na kuongeza kuwa Tume haina pingamizi iwapo wabunge watatunga sheria inayoruhusu makundi hayo kujiandikisha na baadaye kupiga kura.

 

Ozil: Wachezaji Tunapaswa Kulaumiwa
Mkuu wa Wilaya atoa agizo zito makanisani