Kiungo kutoka nchini Ufaransa, N’Golo Kante ameripotiwa kuwa katika mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal katika kipindi hiki cha kuelekea majira ya kiangazi.

Kiungo huyo ambaye ni sehemu ya kikosi cha klabu bingwa nchini England, Leicester City ameonyesha kuwa na mipango hiyo kutokana na kuhusishwa na taarifa za kuondoka King Power Stadium baada ya kumaliza shughuli ya kufikia mafanikio kutwaa taji.

Taarifa zilizochapishwa na jarida la michezo la nchini Ufaransa liitwalo Le 10 Sport, zimeeleza kwamba, Kante anajipanga kucheza soka kaskazini mwa jijini London, kutokana na kuwa na ndoto hizo tangu akiwa na umri mdogo.

Hata hivyo imebainika kwamba Kante mwenye umri wa miaka 25, aliwahi kusema mbela ya watu wake wa karibu, kwamba endapo itatokea anahitaji kuachana na The Foxes, atakua radhi kubaki nchini England na kujiunga na Arsenal.

Maneno hayo yanadaiwa kusemwa na Kante, kufuatia fununu zilizopo za kuwindwa na baadhi ya klabu za soka barani Ulaya, kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha wakati wa msimu wa 2015-16 ambao ulifikia tamati hapo jana.

Mbali na klabu ya Arsenal kuonyesha kuwa tayari kumsajili Kante, klabu nyingine zinazotajwa kuwa katika mawindo ya kuiwania saini ya kiungo huyo ni Chelsea pamoja na Real Madrid.

Serengeti Boys Kupambana Na Wenyeji India
Roy Hogdson Atangaza Kikosi Cha England, Amtema Walcott